Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Friday, 25 March 2016
AZAM YAITWANGA 7 FRENDS RANGERS

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, asubuhi ya leo imeichapa Friends Rangers mabao 7-1 katika mchezo wa kirafiki wa mazoezi uliofanyika katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya benchi la ufundi kuwaangalia na kuwapima wachezaji ambao hawajapata muda mwingi wa kucheza msimu huu pamoja na wale wasiokuwepo katika majukumu ya timu zao za Taifa.
Benchi la ufundi pia lilitumia fursa hiyo kuwajaribu wachezaji wanne wa Azam FC Academy, beki Joshua John, viungo Ferej Khamis ‘Ozil’, Rajabu Odas na mshambuliaji Shaaban Idd, ambao walifanikiwa kuonyesha viwango vizuri.  
Hadi kipindi cha kwanza cha mchezo huo kinamalizika, Azam FC ilikuwa mbele kwa mabao 4-0, yaliyofungwa na Ramadhan Singano ‘Messi’ dakika ya pili kwa mpira wa moja kwa moja wa adhabu ndogo, kabla ya kiungo Michael Bolou kuongeza la pili dakika tatu baadaye kwa shuti kali nje ya eneo la 18.
Mshambuliaji Didier Kavumbagu naye akapiga la tatu dakika ya 37 baada ya kupokea pasi safi ya Messi, dakika sita baadaye kabla ya mpira kwenda mapumziko kiungo Mudathir Yahya aliongeza la nne.
Jumla ya mabao matatu yaliongezeka kipindi cha pili yakifungwa na wachezaji walioingia kipindi hicho, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (dk52), winga Khamis Mcha ‘Vialli’ (dk46) na kinda Shaaban Idd (dk86), huku Allan Wanga akikosa mkwaju wa penalti uliopatikana baada ya Mcha kuangushwa na kipa wa Friends inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Friends Rangers yenyewe ilijipatia bao lao la kufutia machozi dakika ya 73 kupitia kwa nyota wao Cosmas Lewis kwa mkwaju wa penalti baada ya Aggrey Morris kumfanyia madhambi mchezaji mmoja wa Friends ndani ya eneo la 18.
Katika jambo la kufurahisha zaidi, Rangers ilimtumia winga wa Azam FC, Joseph Kimwaga, katika mchezo huo aliyepelekwa kwa mkopo kwenye timu ya Simba, huku pia kikosini kwao ikiwa na wachezaji wengine waliowahi kuwika na kupitia ndani ya Academy ya Azam FC kama vile nahodha wa zamani wa kikosi hicho, Abdul Mgaya.
Azam FC iliyoanza mazoezi jana mara baada ya mapumziko ya siku tatu, katika mchezo huo ilipata pigo dakika ya 36 baada ya kuumia goti kwa beki wake kushoto Gadiel Michael na nafasi yake ikachukuliwa na Wazir Salum ‘Waza’.
Mara baada ya mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Mario Marinica alifurahishwa na viwango vya wachezaji waliocheza mchezo huo akisema kuwa wananafasi ya kufanya vema zaidi uwanjani katika mechi zinazokuja kama wakiendelea kucheza kwa namna hiyo.
Jumla ya wachezaji wa nane wa Azam FC inayodhaminiwa na Benki bora kabisa nchini ya NMB, wameukosa mchezo huo kutokana na kuwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa, saba wakiwa Tanzania ‘Taifa Stars’ na Jean Mugiraneza akiwa Rwanda ‘Amavubi’.
Kikosi cha Azam FC leo:
Mwadini Ally/Ivo Mapunda (dk46), Ramadhan Singano/Rajab Odas (dk61), Gadiel Michael/Wazir Salum (dk36), Pascal Wawa/Aggrey Morris (dk46), Racine Diouf/Abdallah Kheri (dk46), Said Morad/Joshua John (dk61), Frank Domayo/Ferej Khamis (dk61), Michael Bolou/Salum Abubakar (dk46), Mudathir Yahya/Shaaban Idd (dk61), Allan Wanga, Didier Kavumbagu/Khamis Mcha (dk46) 
Read more
ADI KUTOKA ENGLAND KUIONGEZEA NGUVU TAIFA STARS

Mtanzania ADI YUSSUF mzaliwa wa ZANZIBAR yumo nchini akitokea ENGLAND kwenye mji uitwao MASFIELD ambapo kunatimu iitwayo Mansfield Town Football Club hii ndiyo timu anayo tokea huyu MTANZANIA, Ana umri wa miaka 24 kwani alizaliwa 20 February 1992 pia nafasi anayo cheza ni mshambuliaji alianza maisha yake ya soka kwenye timu ya LEICESTER CITY tayari amejiunga na timu ya taifa kuongeza nguvu huenda akalitumikia taifa kwenye mechi ya jumatatu dhidi ya CHAD pale taifa.
Kwa mujibu wa mtandao wa SKY SPORTS nilipokuwa napekenyua undani wa mchezaji huyu msimu huu kwenye mashindano ya Capital One Cup,Sky Bet League,Johnstone's paint na The FA Cup anaidadi ya magoli 5 aliyoifungia timu hiyo inayo shiriki League Two.
Read more
Tuesday, 22 March 2016
TAIFA STARS  YAJINOA HUKO MJINI D'JAMENA.

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’   leo imefanya mazoezi katika uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya ulipo katika jiji la D’jamena ikiwa ni maandalizi ya mchezo dhidi ya wenyeji Chad siku ya Jumatano.
Taifa Stars imefanya mazoezi kuanzia majira ya saa 9 alasiri, ikiwa ni sawa na muda utakaochezwa mchezo siku ya Jumatano sawa na saa 11 kwa saa za nyumbani Tanzania na Afrika Mashariki.
Akiongelea maandalizi ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Taif Stars Charles Boniface Mkwasa amesema anashukuru vijana wake waliotangulia wamefika salama, hakuna majeruhi na wote wameweza kufanya mazoezi aliyoyapangilia.
“Hapa D’jamena hali ya hewa ni joto kali tofauti na nyumbani, kwa hizi siku mbili tutakazofanya mazoezi hapa, naimani vijana wataweza kuzoea hali ya hewa na kufanya vizuri katika mchezo wa Jumatano” alisema Mkwasa.
Mkwasa amesema wachezaji wake wametoka katika vilabu vyao ambavyo vilikua na michezo mwishoni mwa wiki, wote bado wako fit kikubwa wanafanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo.
“Hatujapata muda mrefu wa kufanya mazoezi kwa pamoja, wachezaji walikua na majukumu katika vilabu vyao, nashukuru wote wamewasili wakiwa salama na kesho wataungana na wachezaji wenzao wanaokuja katika kundi la pili kwa ajili ya mazoezi ya mwisho na mchezo wenyewe” aliongeza Mkwasa.
Read more

Labels