#htmlcaption1 KIMATAIFA kwa habari za michezo kutoka nchi mbali mbali duniani MAKALA kwa interview mbali mbali pia mastory mengi kwa njia ya video hapa ni mahal pake BURUDANI Kwa taarifa zinazo husu muziki na mambo mengine yakiburudani
Friday, 25 March 2016
JORDAN YASHINDA 8 CHINI YA REDKNAPP

Timu ya taifa ya Jordan ilipata ushindi mkubwa wa mechi yao ya kwanza chini ya meneja wao mpya wa muda Harry Redknapp.
Timu hiyo ililaza Bangladesh 8-0 kwenye mechi ya kufuzu Kombe la Dunia iliyochezwa Alhamisi uwanja wa Amman.
Mshambuliaji wa klabu ya Al-Kuwait Hamza Al-Dardour alifunga mabao matatu kipindi cha kwanza na kusaidia vijana hao wa Redknapp kuongoza 5-0 wakati wa mapumziko.
Jordan wamo nambari mbili katika kundi B lenye mataifa matano, wakiwa alama mbili nyuma ya Australia, ambao wanawasubiri mjini Sydney tarehe 29 Machi.
Watahitajika kulaza Socceroos ili kufika raundi ya tatu ya kufuzu kwa fainali za Urusi mwaka 2018 katika bara Asia.
Redknapp, aliyekuwa meneja wa Tottenham, alikubali kuwaongoza Jordan kwa mechi mbili za mwisho za kundi lao.
Mapema wiki hii hata hivyo alisema yuko radhi kuendelea kuwakufunza.
Read more
AZAM YAITWANGA 7 FRENDS RANGERS

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, asubuhi ya leo imeichapa Friends Rangers mabao 7-1 katika mchezo wa kirafiki wa mazoezi uliofanyika katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.
Mchezo huo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya benchi la ufundi kuwaangalia na kuwapima wachezaji ambao hawajapata muda mwingi wa kucheza msimu huu pamoja na wale wasiokuwepo katika majukumu ya timu zao za Taifa.
Benchi la ufundi pia lilitumia fursa hiyo kuwajaribu wachezaji wanne wa Azam FC Academy, beki Joshua John, viungo Ferej Khamis ‘Ozil’, Rajabu Odas na mshambuliaji Shaaban Idd, ambao walifanikiwa kuonyesha viwango vizuri.  
Hadi kipindi cha kwanza cha mchezo huo kinamalizika, Azam FC ilikuwa mbele kwa mabao 4-0, yaliyofungwa na Ramadhan Singano ‘Messi’ dakika ya pili kwa mpira wa moja kwa moja wa adhabu ndogo, kabla ya kiungo Michael Bolou kuongeza la pili dakika tatu baadaye kwa shuti kali nje ya eneo la 18.
Mshambuliaji Didier Kavumbagu naye akapiga la tatu dakika ya 37 baada ya kupokea pasi safi ya Messi, dakika sita baadaye kabla ya mpira kwenda mapumziko kiungo Mudathir Yahya aliongeza la nne.
Jumla ya mabao matatu yaliongezeka kipindi cha pili yakifungwa na wachezaji walioingia kipindi hicho, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (dk52), winga Khamis Mcha ‘Vialli’ (dk46) na kinda Shaaban Idd (dk86), huku Allan Wanga akikosa mkwaju wa penalti uliopatikana baada ya Mcha kuangushwa na kipa wa Friends inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL).
Friends Rangers yenyewe ilijipatia bao lao la kufutia machozi dakika ya 73 kupitia kwa nyota wao Cosmas Lewis kwa mkwaju wa penalti baada ya Aggrey Morris kumfanyia madhambi mchezaji mmoja wa Friends ndani ya eneo la 18.
Katika jambo la kufurahisha zaidi, Rangers ilimtumia winga wa Azam FC, Joseph Kimwaga, katika mchezo huo aliyepelekwa kwa mkopo kwenye timu ya Simba, huku pia kikosini kwao ikiwa na wachezaji wengine waliowahi kuwika na kupitia ndani ya Academy ya Azam FC kama vile nahodha wa zamani wa kikosi hicho, Abdul Mgaya.
Azam FC iliyoanza mazoezi jana mara baada ya mapumziko ya siku tatu, katika mchezo huo ilipata pigo dakika ya 36 baada ya kuumia goti kwa beki wake kushoto Gadiel Michael na nafasi yake ikachukuliwa na Wazir Salum ‘Waza’.
Mara baada ya mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Mario Marinica alifurahishwa na viwango vya wachezaji waliocheza mchezo huo akisema kuwa wananafasi ya kufanya vema zaidi uwanjani katika mechi zinazokuja kama wakiendelea kucheza kwa namna hiyo.
Jumla ya wachezaji wa nane wa Azam FC inayodhaminiwa na Benki bora kabisa nchini ya NMB, wameukosa mchezo huo kutokana na kuwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa, saba wakiwa Tanzania ‘Taifa Stars’ na Jean Mugiraneza akiwa Rwanda ‘Amavubi’.
Kikosi cha Azam FC leo:
Mwadini Ally/Ivo Mapunda (dk46), Ramadhan Singano/Rajab Odas (dk61), Gadiel Michael/Wazir Salum (dk36), Pascal Wawa/Aggrey Morris (dk46), Racine Diouf/Abdallah Kheri (dk46), Said Morad/Joshua John (dk61), Frank Domayo/Ferej Khamis (dk61), Michael Bolou/Salum Abubakar (dk46), Mudathir Yahya/Shaaban Idd (dk61), Allan Wanga, Didier Kavumbagu/Khamis Mcha (dk46) 
Read more
DUNIA ITAKUKUMBUKA NGULI JOHAN CRUYFF

Nguli wa soka wa Kidachi alifariki dunia Alhamisi akiwa na umri wa miaka 68, lakini kazi zake zitadumu daima na hakuna mwenye ushawishi kama wake zaidi ya miaka 50 iliyopita
Amekwenda, lakini kazi zake zitadumu milele. Johan Cruyff alibadili soka: kama mchezaji, kocha, mshauri na moja wa wanazuoni wakubwa wa soka, Mdachi huyu ameacha urithi utakaodumu siku zote. Alifanya mageuzi ya soka katika zama za kileo.

Cruyff alipenda kuwa tofauti. Alilenga kufanikiwa kama mchezaji mdogo kwani baba yake alifariki akiwa mdogo sana, Johan akiwa mdogo (akifahamika kwa jina la kuzaliwa Hendrik Johannes) alikuza ujuzi wake na kuwa mchezaji mahiri.

Mama yake alifanya kazi kama mfanya usafi wa Ajax na baba yake wa kambo alikuwa mfanya kazi wa klabu ya Amsterdam. Hivyo Cruyff alijifunza thamani ya kufanya kazi kwa bidii akiwa na umri mdogo na alikuwa akivifanyia kazi kwa juhudi nyingi vipaji vyake, alijiunga na akademi ya Ajax na akawa mchezaji bora zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Cruyff aliiongoza Ajax kutwaa vikombe vitatu vya Kombe la Ulaya na alitwaa tuzo ya Ballon d'Or mara tatu pia. Chini ya mwana mapinduzi Rinus Michels, Johan alikuwa mchezaji hatari zaidi wa kipindi chake. Total Football Na kwa pamoja wawili hao waliiongoza Uholanzi kutinga fainali ya Kombe la Dunia 1974 - ambapo waliishia kufungwa na Ujerumani Magharibi mjini Munich.

Licha ya kipigo hicho, walikonga nyoyo za mashabiki wote wa soka duniani kwa uchezaji wao kushirikiana.

"Tumepoteza moja ya mchezo muhimu sana katika maisha yetu, lakini nadhani hilo limetupatia umaarufu ambao huenda tusingeupata kama tungekuwa tumeshinda," alisema baadaye. "Kwa sababu watu walitaka tushinde, jambo hilo lilivuta usikivu wa wengi, na upendo. Kwa muda wa majuma manne katika michuano hii hakuna aliyekuwa akizungumzia kushinda ama kufungwa - hadhira ya ulimengu ilitaka kuona kandanda safi likichezwa. Kwa hiyo si kwamba tunajitetea, ni kweli - matokeo ya fainali hayaniumizi sana."


Uholanzi walipoteza fainali ya 1978 pia, lakini kipindi hiki Cruyff hakuwepo. Aliamua kuyakosa mashindano kwa sababu zake binafsi; lakini alikuwa akijiandaa kwa ajili ya sehemu yake mpya : Barcelona. 
Ajax walitaka kumuuza kiungo huyo Real Madrid, lakini Cruyff alikuwa na mtazamo tofauti.
"Nakumbuka safari yangu kwenda Hispania ilikuwa na mikingamo mingi," alisema. Watu walisema nilikuwa nikienda kwenye nchi ya kifashisti. Rais wa Ajax alitaka kuniuza Real Madrid. Lakini nilizaliwa muda mfupi tu baada ya vita na nilifundishwa kutokukubali mambo kiholela. Barcelona hawakuwa katika kiwango walichokuwa nacho Real Madrid kisoka, lakini ilikuwa ni changamoto kuichezea klabu ya Catalan, Barcelona ilikuwa zaidi ya klabu."
Na ikiwa na Cruyff ilikuwa klabu kubwa zaidi. Mwaka wake wa kwanza Camp Nou ulikuwa mzuri kwani walishinda ubingwa wa La Liga kwa mara ya kwanza tangu 1960, wakiifunga Real Madrid 5-0 msimu huo na kuweka alama yao iliyodumu hadi hivi leo.

Kipindi chake chote alichodumu Catalunya hakikuwa na mafanikio sana, lakini alikuwa mshauri wa rais Josep Lluis Nunez kabla ya kuondoka. Cruyff alimtaka mkurugenzi wa klabu kuunda akademi yenye mfumo wa Ajax na kukuza wachezaji wenye vipaji kama yeye alivyotokea Amsterdam. Aliamini wakifanya hivyo wangeweza kushindana vizuri na Real Madrid.

Mara nyingi Cruyff alikuwa akienda Marekani, akarejea tena La Liga akiwa na Levante na aliiongoza Feyenoord kutwaa taji katika nchi yake ya nyumbani.  


Aliporejea Barcelona kuendelea na kazi ya ukocha aliyoianza kwa mafanikio Ajax, kilikuwa tena ni kipindi cha utawala wa Real Madrid. Cruyff aliwasili mnamo 1988, Nunez aliamini kumrejesha mdachi huyo kungebadili mambo yote -  na alikuwa sahihi.

Ilichukua muda lakini wachezaji wadogo walikuwa wakitokea kwenye timu ya vijana na Cruyff aliwaunganisha na wachezaji bora wa dunia. Timu ya ndoto ya wengi ilizaliwa, ikashinda taji la La Liga mfululizo kati ya mwaka 1991 na 1994, hali kadhalika na Kombe la Ulaya. Ghafla Barca hawakuwa chini ya kivuli cha Madrid tena.

Wiki moja baada ya kurejea klabuni, Cruyff alikwenda kuangalia timu ya vijana, akamwona kinda Pep Guardiola akicheza kama kiungo wa kulia. Alimtaka mchezaji mwenzake wa zamani Carles Rexach kumuingiza Pep kati kipindi cha pili ili acheze sehemu muhimu zaidi. Aliimudu nafasi hiyo mara moja na punde akaingizwa kwenye kikosi cha kwanza.

Guardiola alikuwa kocha wa Cruyff dimbani na Pep alizivuta nyuzi vilivyo katika timu iliyokuwa imesheheni vipaji kipindi hicho, ilikuwa ni Barca yenye mafanikio mno katika historia.

Baadaye katika utawala wake, Cruyff aliungua shinikizo la moyo na alishauriwa kuacha kazi ya ukocha na daktari wake. Alipoondoka 1996, hakufanya kazi nyingine lakini bado alikuwa na ushawishi.

Akirejea tena kama mshauri wa Joan Laporta, alipendekeza kuteuliwa kwa Frank Rijkaard mnamo 2003. Kwa mara nyingine tena Barca walipata mafanikio, wakitwaa mataji ya ligi na Ligi ya Mabingwa Uefa 2006.

Lakini tena bado kulikuwa na mengi zaidi. Baada ya kushindwa kufanya vizuri kwa kiwango fulani, Laporta aliponea tundu la sindano na kikosi kilihitaji kuimarishwa tena. Rijkaard aliondoka klabuni, ingawa Jose Mourinho alikuwa akitamani kibarua hicho Camp Nou, Cruyff alimchagua Guardiola.

Wengi walimsonda kidole kwa kudai kuwa hana uzoefu wa kazi ya ukocha, lakini Mdachi alisema: "Kipimo kikubwa kwa kocha katika timu kama Barca ni nguvu ya kufanya maamuzi na uwezo wa kuzungumza kwenye vyombo vya habari, kwa sababu huo ndio uongozi. Baada ya hapo ni rahisi kwa wale wanaojua soka. Lakini si wengi wanaofahamu." 





Na Guardiola alijua. Kutoka kwa Michels kwa Cruyff na Johan akampa Pep Guardiola na Barca ikaibuka kuwa na mafanikio makubwa kuliko kipindi chote cha historia yao, wakitwaa mataji yote sita ndani ya msimu mmoja chini ya nahodha wa zamani aliyefanya hayo makuu ndani ya miezi 18 kama kocha. Na 2010 Hispania ikiwa na timu yenye asilimia kubwa ya wachezaji wa Barcelona iliibuka bingwa wa michuano ya Kombe la Dunia kwa kuifunga Uholanzi na kumwachia Cruyff kumbukumbe ambayo hakuisahau - ingawa alifurahishwa zaidi na mfumo waliotumia La Roja.
"Huu ni mfumo hatari na mbaya sana, unakamata macho na kupumbaza kabisa akili, mfumo mgumu wa soka, uliwafanya Waholanzi wasiweze kuifunga Hispania," alisema baada ya mechi. "Kama kwa mchezo huu walipata haja ya moyo wao, ni vema. Lakini wamepoteza. Wamecheza kinyume cha soka."

Cruyff amekuwa akizungumzia mfumo daima na kama alivyosema kuhusu kufungwa kwa Uholanzi 1974, amesisitiza kuwa anaiheshimu falsafa ya mpira kuliko kuogopa kufungwa. Kwake mfumo ni jambo la msingi zaidi.

Mnamo Alhamisi, mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 68 alishindwa vita na Saratani, lakini mfumo wake wa kipekee utakumbukwa milele, na soka lenyewe kwa kiasi kikubwa linamshukuru sana Johan Cruyff.

Mbunifu, na mwana mitindo, mwelimishaji, mchezaji soka mahiri, kocha bora, Mwanafalsafa na kila sifa katika soka la ulimwengu wa kisasa, Cruyff ameondoka lakini timu aliyoisaidia kutawala soka la dunia na penalti yake maarufu ya pasi aliyopiga 1982 ilirudiwa tena na Lionel Messi na Luis Suarez.

"Watoto wanahitaji msaada kutoka kwetu" alikiambia Goal katika mahojiano rasmi ya 2009. "Nilijielimisha mwenyewe mitaani. Niliendesha baiskeli, nilicheza soka, nilikimbia nikifanya kila kilichowezekana, lakini leo nipo kwenye gari na hakuna sehemu ya kucheza mtaani. Hivyo inabidi nibuni kitu kingine tofauti. Mwili unaozaliwa nao ndio unaokufa nao. Naam unaweza kubadili mambo machache lakini si kila kitu. Leo magari, kompyuta na mtandao wa intaneti na kila kitu mazoezi ya viungo hayana nafasi tena na soka pekee ndilo linaloweza kukupa mazoezi."

Kila alichofanya, Johan Cruyff alipambana kuleta tofauti. Jinsi gani atakumbukwa.
Read more
ADI KUTOKA ENGLAND KUIONGEZEA NGUVU TAIFA STARS

Mtanzania ADI YUSSUF mzaliwa wa ZANZIBAR yumo nchini akitokea ENGLAND kwenye mji uitwao MASFIELD ambapo kunatimu iitwayo Mansfield Town Football Club hii ndiyo timu anayo tokea huyu MTANZANIA, Ana umri wa miaka 24 kwani alizaliwa 20 February 1992 pia nafasi anayo cheza ni mshambuliaji alianza maisha yake ya soka kwenye timu ya LEICESTER CITY tayari amejiunga na timu ya taifa kuongeza nguvu huenda akalitumikia taifa kwenye mechi ya jumatatu dhidi ya CHAD pale taifa.
Kwa mujibu wa mtandao wa SKY SPORTS nilipokuwa napekenyua undani wa mchezaji huyu msimu huu kwenye mashindano ya Capital One Cup,Sky Bet League,Johnstone's paint na The FA Cup anaidadi ya magoli 5 aliyoifungia timu hiyo inayo shiriki League Two.
Read more
Thursday, 24 March 2016
JOHNSON NA WACHEZAJI WENGINE WA KIINGEREZA  WALIO LALA LUMANDE

Baada ya muingereza Adam Johnson kukutwa na hatia ya kutembea na binti mdogo ambaye umri wake upo chini ya miaka 18 hukumu nayo imeshapita atatumikia kifungo cha miaka 6 gerezani hili sio tukio la kwanza kwa wachezaji wa kiingereza nimekuandalia orodha ya wachezaji wa kiingereza walio fungwa kwa makosa ya mbali mbali;-

JOEY BARTON
huyu jamaa kwanza sifa yake kubwa ni mtukutu yeye ni siku 77 alifungwa 2007 kutokana na vurugu alizozifanya kwenye jiji la MANCHESTER.

TONY ADAMS
beki wa Arsenal Tony Adams alikuwa jela kwa miezi minne mwaka 1990 baada ya yeye kuendesha gari akiwa ametumia pombe .

DUNCAN FERGUSON
miezi mitatu jela mwaka 1995 kwa kumshambulia John McStay wa Raith Rovers wakati alipokuwa akiichezea Rangers.
alijiunga na Newcastle mwaka 1998 lakini akarudi Everton baada ya mwaka mmoja tu. Yeye alistaafu soka Goodison Park mwaka 2006.

Lee Hughes
Huyu yeye alikuwa anaendesha gari ovyo na kupelekea kusababisha kifo cha Douglas Graham hii ilikuwa Agosti 2004 hata hivyo timu yake kwa kipindi hicho West Bromwich Albion ilimtimua kazi mshambuliji huyo na hukumu ilipo pita ni miaka 6 alifungwa.
Luke McCormick

Miezi minne jera kwa kosa la kusababisha ajari alikuwa ni kipa wa Plymouth ilikuwa ni Julai 2008.
Wapo wengi wenye matukio ya ajabu wengine ni 
Marlon King 
 Ched Evans
Read more
MC HALE KUVAANA NA SERENA


Mcheza Tenesi Christina Mc Hale raia wa Marekani amemshinda Misaki Doi wa japani katika michuano ya wazi ya Miami.
Mchale alishinda kwa jumla ya seti 6-2 kisha akapoteza kwa 4-6 na kumaliza na ushindi wa seti 7-5,katika raundi ya mwisho.
Kwa ushindi huo nyota huyu wa tenesi atachuana na nyota namba moja wa kwa ubora wa mchezo huo Serena Williams, katika raundi inayofuata.
Katika raundi nyingine Mfaransa Alize Cornet alimshinda Galina Voskoboeva wa Kazakhstan hivyo mfaransa huyu atachuana na Agnieszka Radwanska, huku Julia Goerges wa Ujerumani akimshinda Nao Hibino wa Japani na hivyo atacheza na Samantha Stosur raia wa Austalia katika mchezo unaofuata.
Read more